We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 3, 2019

Makonda uso kwa uso na Mahiga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo September 03, amemkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga muswada wa mapendekezo wa marekebisho ya sheria ya mirathi kwa ajili ya kufanyiwa maboresho na kuwasilishwa bungeni.

Muswada huo umewasilishwa mjini Dodoma na kuzitaja sheria kandamizi ambazo angependa zifanyiwe marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya kiserikali ya mirathi, Sheria ya Mirathi ya Kimila pamoja na  Sheria ya Mirathi ya Kidini kwa madai ya kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa zikileta mateso kwa wajane.
Makonda amekuwa akipigia kelele yafanyiwe maboresho pamoja na kipengele cha kumpa uhalali mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala mali kuhamishwa, pamoja na usawa wa watoto.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa alichokifanya Makonda ni ushujaa wa hali ya juu na ameweka historia ya jambo ambalo halijawahi kufanyika na kuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list