'MADINI HAYA YANA MADHARA MAKUBWA’-KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI LEO
Leo kutoka bungeni Dodoma moja ya mambo ambayo yameendelea ndani ya bunge hilo ni pamoja na uwasilishwaji wa maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuhusu Azimio la Kuridhia Mkataba wa Minamata Kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury ambapo azimio hilo limepitishwa na bunge hilo. Awali msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ofisi ya makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) aliwasilisha maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuhusu Azimio hilo na kueleza kwa kina kuhusu madhara ya zebaki.
Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya
No comments:
Post a Comment