We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 11, 2019

Kagere sio majeruhi, kuiwahi Mtibwa Sugar

Taarifa za mshambuliaji kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba Meddie Kagere kuwa majeruhi hazina ukweli wowote kwani jana aliitumikia Rwanda kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia
Katika mchezo huo Kagere alipachika mabao mawili
Kagere anatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi hivyo kuuwahi mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Ijumaa
Kitakachomfanya Kagere asicheze mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar labda uchovu, kocha Patrick Aussems aamue kumpumzisha
Hata hivyo Aussems amekuwa akimuandaa winga Deo Kanda kucheza nafasi ya ushambuliaji wa kati
Simba imebaki na mshambuliaji mmoja tu (Kagere) baada ya Bocco na Wilker Da Silva kuumia
Bocco ameanza mazoezi mepesi jana lakini atahitaji siku kadhaa kuimarika kabla ya kurejea dimbani
Huenda kazi ya kwanza ya usajili ya CEO mpya wa Simba Senzo Mazingisa ikawa kusajili mshambuliaji wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi ujao

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list