We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

Kagera sugar watamba kuifunga Simba Kaitaba

Baada ya kupata ushindi mara mbili mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema wataendelea kuifunga Simba katika mchezo unaofuata.
Kagera Sugar wanatarajia kukutana na Simba Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Msimu uliopita, Kagera Sugar iliifunga Simba michezo yote miwili ambayo ilipata ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani na ilishinda bao 1-0 iliporudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Mexime alisema wanaendelea kujipanga na malengo yake ni kuendelea kuifunga Simba, hata kama wataanzisha wachezaji wote wa kigeni.
Alisema pamoja na Simba kuwa na wachezaji wengi wa kigeni ambao wana viwango vizuri uwanjani, lakini hawawezi kupata pointi tatu kutoka kwao.
"Hata kama Kocha wa Simba (Patrick Aussems) ataamua kuwaanzisha wachezaji wake wote wa kigeni haitotusumbua, kwani lazima tuwafunge na rekodi zinajieleza," Mexime aliliambia 
Bingwa
"Kile kilichotokea msimu uliopita tuliwafunga nyumbani na ugenini, lazima msimu huu kijirudie, Simba watazionea timu nyingine si Kagera Sugar ikiwa chini yangu"alisema Mexime.
Tayari Kagera Sugar imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, kisha ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance, wakati Simba ilianza ligi hiyo kwa kuifunga JKT Tanzania mabao 3-1 na baadae ilitoa kipigo cha mabao 2-1 kwa Mtibwa Sugar
Timu zote zina alama sita na tofauti ya mabao matatu ya kufunga na kufungwa
Katika misimu mitatu iliyopita, Simba imeifunga Kagera Sugar mara mbili tu wakati timu hiyo imeshinda michezo minne

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list