We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

Askofu Gwajima aungana na RC Makonda

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, ameunga mkono  kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, iliyowaomba viongozi wa dini kwenda kutoa mahubiri nyakati za usiku katika kumbi mbalimbali za starehe.


Akizungumza leo Septemba 17 na EATV&EA Radio Digital, Askofu Gwajima amesema kuwa, yeye binafsi yuko tayari kufanya hivyo kwa sababu neno la Mungu linapaswa lihubiriwe maeneo yote na liwafikie watu wote.
''Injili ya Yesu inatakiwa ihubiriwe kila mahali, iwe kwa wavuta bangi, iwe kwa wanaokunywa Pombe, alichokisema RC ni kile kimeandikwa kwenye Biblia, hivyo ni jambo zuri watu kuhubiriwa habari za Yesu ili wasije kusema hawakusikia, na mimi niko tayari ukiniita mahali kwamba nije nihubiri, naenda popote pale'' amesema Gwajima.
Makonda alitoa kauli hiyo Septemba 8, 2019, wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtume Mwamposa na aliahidi kutoa kibali kwa mtumishi yeyote, atakayekuwa tayari kueneza Injili katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list