We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 18, 2019

Hivi ndivyo Liverpool, Chelsea Walivyopigwa Ligi ya Mabingwa Ulaya ( VIDEO )

LIGI ya Mabingwa Ulaya kwa hatua ya makundi ya 2019/2020 imeanza jana Septemba 17, 2019, kwa kushuhudia rekodi mbalimbali zikiwekwa ambapo bingwa mtetezi, Liverpool, amefungwa katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Napoli  kwa mabao 2-0 ugenini.
Chelsea wakiwa nyumbani wamekosa penati na kukubali kichapo cha bao 1-0 utoka kwa Valencia.
Jumla ya magoli 21 yalifungwa katika mechi nane zilizochezwa usiku wa jana ikiwa ni idadi kubwa katika mechi za ufunguzi.
Katika michuano hiyo, Mbwana Ally Samata nahodha wa Taifa Stars ameingia katika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano hiyo mikubwa  na yenye fedha nyingi.

Pia amekuwa Mtanzania wa kwanza kufunga bao katika michuano hiyo akifunga moja kati ya mabao mawili waliyopata Genk katika kipigo cha mabao 6-2.

Genk imekuwa moja kati ya timu zilizofungwa mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza maana mpaka mapumziko walishafungwa bao 5-1 na mechi ikaisha kwa kufungwa bao 6-2.

Erling Braut Haaland amefunga ‘hat-trick’ katika mechi yake ya kwanza katika mashindano hayo ndani ya dakika 45 akiichezea Salzburg katika ushindi wa mabao 6-2 walioupata dhidi ya Genk.

Lionel Messi amerejea baada ya kuwa majeruhi na kukaa muda amrefu nje ya uwanja, Barcelona wakinusurika kichapo nyumbani kwa Dortmund ambapo kipa wa Barca,  Marc-AndrĂ© ter Stegen,  akipangua penati ya Marco Reus

Ansu Fati amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Barcelona katika michuano hiyo akianza katika mechi ya jana dhidi ya Borrussia Dortmund akiwa na umri wa miaka 16 na siku 351.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list