Zesco United imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuifunga Yanga mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Levy Mwanawasa
Jesse Were aliitanguliza Zesco kwenye dakika ya 25 akitumia makosa ya Ally Ally aliyechelewa kukaba
Hata hivyo Sadney Urikhob aliisawazishia Yanga kwenye dakika ya 30 akimalizia vyema mpira baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Zesco
Kipindi cha pili Yanga ilicheza kwa tahadhari zaidi wakilazimika kukabiliana na presha ya Zesco waliokuwa wakishambulia kwa muda mwingi
Bao la kujifunga la Abdulaziz Makame 'Bui' kwenye dakika ya 79 lilivuruga ndoto za Yanga kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo
Yanga ilipata pigo zaidi kwenye dakika za majeruhi baada ya beki kisiki Lamine Moro kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano
Yanga sasa inahamia kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambako inasubiri kupangiwa mpinzani
Ushindi katika hatua hiyo utawapa nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo
No comments:
Post a Comment