We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 18, 2019

Fatma Karume azungumzia kauli ya Makonda

Wakili wa kujitegemea na aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Fatma Karume, ameonesha kushangazwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, iliyoeleza kinachomuweka madarakani ni njaa tu na kusema kwamba, kiongozi huyo inaonesha ni kwa namna gani hawezi


Akizungumza leo Septemba 18, 2019 na EATV&EA Radio Digital, Fatma Karume amesema kuwa kwa kiongozi yeyote aliyepewa jukumu la kuhudumia wananchi, hakupaswa kutanguliza maslahi yake binafsi.
''Mimi nilikuwa nategemea kwamba, mtu anaingia katika utumishi wa Umma kwa ajili ya huduma kwa wananchi, sasa ukikubali kufanya kazi kama RC na umepewa kazi hiyo na Rais ni kwamba uko  tayari kuwahudumia wananchi, lakini kwa maneno aliyoyasema Makonda yeye yupo pale kujihudumia mwenyewe na njaa zake'' amesema Fatma Karume.
Aidha Wakili huyo ameongeza kuwa,kutokana na kauli hiyo, Makonda ameudhihirisha Umma kwamba hauwezi kusimama peke yake.
''Tatizo ni kwamba yupo pale kujihudumia njaa zake kwa maana huyu mtu hawezi kusurvive bila Serikali na anaitegemea Serikali na nguvu za wananchi ili ale, siyo yeye anayetaka awahudumie Wananchi bali anataka Wananchi wamhudumie yeye kitu ambacho hakiwezekani'' amesema Wakili huyo.
Kauli ya njaa ya  Makonda imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais Magufuli, alipotembelea machinjio ya Vingunguti na kuonesha kutoridhishwa na ujenzi wa machinjio mapya, ambapo alimuagiza Mkuu wa Mkoa kuhakikisha anasimamia miradi ya mkoa wake na inatekelezeka kwa muda muafaka.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list