We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 11, 2019

DC Sabaya awaweka ndani wahasibu

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ameagiza wahasibu wa Chuo cha Ualimu Moshi pamoja na Wakala wa Benki ya CRDB Wilayani humo, kukamatwa mara baada ya kugundua ubadhilifu mkubwa wa shilingi milioni 78 zilizokuwa zinalalamikiwa na Wanafunzi Chuoni hapo.

Akizungumza leo Septemba 11 na EATV&EA Radio Digital, DC Sabaya amesema kuwa mara baada ya kukutana na wote waliotajwa kuhusika na upotevu wa pesa hizo ikiwemo Bodi ya Shule, CRDB pamoja na Mawakala wa ELCT SACCOS, aliagiza wakae ili kuweza kubaini na kujiridhisha kiasi halali kilichopotea.
''Tumekubaliana kwamba wahusika wa wizi huo, huyu Muhasibu wa Chuo na yule Wakala watawajibika kulipa hicho kiasi kwa sababu nao watakuwa sehemu ya uchunguzi huo, lakini ili wasiharibu uchunguzi, nimeagiza wote wakamatwe kwahiyo wote wawili wako ndani mpaka wasubiri kesho saa 5:00 Asubuhi, watanipa majibu ya kilichofikiwa na tutaamua namna ya ulipaji wa fedha hizo ili Wanafunzi waendelee kubaki hapo Shuleni'' amesema DC Sabaya.
Wanafunzi wa Chuo hicho waliandamana siku ya Jumatatu ya Septemba 9 na kushinikiza Serikali kuingilia kati sakata la utapeli wa zaidi ya Sh.milioni 75 za malipo ya ada ambazo hazionekani kwenye akaunti ya Chuo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list