Kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana amerejea kikosini kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya ZESCO United
Bigirimana amekuwa nje kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha ya nyama za paja
Tangu alipotua Yanga, Bigirimana amekuwa akisumbuliwa na majeraha hayo
Wakati Yanga ilipoweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Zesco, Bigirimana aliachwa Dar kuendelea na matibabu
Kurejea kwake huenda kutaongeza 'kitu' kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo bado haijapata makali

No comments:
Post a Comment