Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameutaka uongozi wa timu hiyo uongeze mshambuliaji wakati usajili wa dirisha dogo
Aussems amesema kuumia kwa washambuliaji wake, kunafanya safu yake iwe kwenye mashaka
Kwa sasa Simba inamtegemea mshambuliaji mmoja tu Meddie Kagere wakati nahodha John Bocco na Wilker Da Silva wakiwa majeruhi
Aidha Mbelgiji huyo amesema analazimika kumbadilishia majukumu winga Miraji Athumani
Aussems amesema anahofia kama Kagere atapata majeraha, watakuwa kwenye wakati mgumu sana
"Niliwaambia viongozi tunahitaji kusajili mshambuliaji mwingine, kama Kagere ataumia, basi labda mimi ndio niingie kucheza," amesema
"Nasubiri uongozi chini ya Mtendaji mpya, nna matumaini watalikamilisha hilo mapema"
No comments:
Post a Comment