We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, September 12, 2019

Amuneke alishtaki shirikisho la soka Tanzania Fifa


Kocha aliyeipeleka Tanzania kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2019, Emmanuel Amuneke aliyetimuliwa mara baada ya fainali hizo zilizofanyikia nchini Misri, amelishtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la mchezo huo  Duniani (FIFA) akilalamika kutolipwa stahiki zake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mitandao ya completesports.com na punching.com, Kocha huyo Mnigeria ameamua kupeleka shauri hilo FIFA ili waweze kulitatua.
"Nimewasiliana na FIFA juu ya hilo jambo. Sio suala la kupigia kelele, lakini nina imani watalitazama na kuamua kama ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi," alisema Amuneke.
Amuneke aliyekuwepo hapa nchini tangu alipovunjiwa mkataba Julai mwaka huu, inadaiwa amerejea Hispania ambako ndiko makazi yake ya kudumu yalipo.
TFF walifikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Amuneke baada ya Taifa Stars kufanya vibaya katika  fainali hizo za Afcon 2019 zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.
Katika fainali hizo, Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa pia na timu za Senegal, Kenya na Algeria baada ya kupoteza mechi zote tatu, ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara nane na yenyewe kufunga mawili
Algeria ndio waliobeba taji hilo kwa kuifunga Senegal katika fainali kali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list