We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, September 2, 2019

Amshambulia EX wake, sababu anaolewa na mwingine

Mkulima wa Kijiji cha Nangaru, mkoani wa Lindi Abdallah Shaibu Nyuki (30), amehukumiwa na Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, kwenda jela miaka 8, baada ya kupatikana na makosa 2 ya kutaka kuuwa bila kukusudia.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Mfawidhi Mkuu wa Mahakama hiyo Joel Paul Ngwembe,  amesema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kwanza la kujaribu kuuwa na miaka 4 tena kwa kosa la kujeruhi.
Awali Mwanasheria wa Serikali, Emmanuel John amesema kuwa mshtakiwa akiwa na panga mkononi Disemba 08, 2018, aliwashambulia Hashimu Bakari Mnocho na Zakia Salum Kindumba, ambaye ni mwanamke aliyeachana naye, baada ya kuwakuta wako pamoja wakizungumzia mipango ya ndoa.
Mwanasheria huyo amesema kuwa baada ya kuwakuta wakiwa wanazungumza mshtakiwa akiwa na panga mkononi aliwajeruhi kwa kuwashambulia mwilini, ambapo baada ya kufanya tukio hilo alikimbia Kijiji cha jirani.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list