We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 3, 2019

Amkeni Bwana....wamerudiana wana!!

Ni takribani siku 4 zimepita tangu kuachiwa kwa wimbo wa pamoja Nandy na Billnas unaokwenda kwa jina la Bugana, ambapo ndani ya siku hizo hizo 4 umeweza kutazamwa na watu zaidi ya laki 5.

Wimbo wa pamoja kati ya Nandy na Billnas umeondoa taswira ambayo ilikuwepo kwa mashabiki wengi, ambao walikuwa wakiamini kuwa wasanii hao ambao wamewahi kuwa wapenzi hawana maelewano.
Kupitia Instagram zao wamekuwa wakiweka picha kadhaa huku zikiambatana na maneno ambayo yamekuwa yakionesha uchokozi, huku mashabiki wengi wakitoa maoni yao kuonesha watu hao huenda wapo pamoja.
Mojawapo ya 'Post' ambayo imepata Komenti nyingi, imewekwa na Nandy akiwa na Billnas kisha kuandika "Eti tunafanana na bro wangu?????"
Katika komenti wengi wameonesha kupinga hilo huku wengine wakitumia lugha kali, kejeli na kuwadhihaki wawili hao huku wakiitaja mara kwa mara video yao ya pamoja ambayo iliwahi kuvuja.
"Bro tena Nandy kwa 'kiss' lile jamani tuoneeni huruma basi mnatuchanganya," aliandika shabiki.
"Nandy unajua kuvuruga watu," aliandika shabiki mwingine.
Kwa mujibu wa Nandy na Billnas wanasema kwa sasa ni marafiki wa kawaida na ukaribu ambao watu wanauona NI kwaajili ya kibiashara zaidi lakini mashabiki wengi hawakubaliani na hilo.
"AMKENI BWANA ....WAMERUDIANA," aliandika shabiki mwingine

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list