Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar hautakuwa mwepesi kutokana na timu hiyo kuwa ngumu kufungika inapocheza uwanja wake wa nyumbani
Hata hivyo amesema amekiandaa kikosi chake vyema kukabiliana na upinzani wowote utakaojitokeza kwenye mchezo huo lengo likiwa kushinda
"Tumefanya mazoezi ya kutosha kwa siku mbili kabla ya kuja Kagera hivyo tumejipanga vizuri japokuwa mchezo utakuwa mgumu," alisema Aussems baada ya mazoezi ya Simba yaliyofanyika uwanja wa Kaitaba
Kagera Sugar imeshinda michezo yote mitatu iliyopita dhidi ya Simba kwenye ligi
Mwenendo huo umeifanya timu hiyo ijiamini kila inapokutana na Simba na hivyo kufanya michezo baina ya timu hizo kutotabirika
Simba ilitua Kagera jana ikiwa na kikosi cha wachezaji 22
Nahodha John Bocco, Gadiel Michael na Clatous Chama wameachwa jijini Dar es salaam kutokana na majeruhi

No comments:
Post a Comment