We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, September 12, 2019

Alichokisema Ngeleja kuhusu kumuomba msamaha Magufuli ( VIDEO )




Mbunge wa Sengerema William Ngeleja amesema kuwa, amefurahishwa na hatua za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kumsamehe yeye pamoja na wabunge wengine.

William Ngeleja
Ngeleja amesema kupitia msamaha huo, amepata faraja kwa kuamini kuwa msamaha huleta faraja kwa maisha ya mwanadamu.
Ngeleja ameyabainisha hayo leo Septemba 12 katika kikao cha Bunge mjini Dodoma, ambapo amepata fursa ya kumshukuru  Rais Magufuli kwa hatua hiyo aliyoifanya dhidi yao, hii ni baada ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kuwapongeza kwa hatua ya kumuomba radhi Rais Magufuli.
''Mimi natumia nafasi hii na kwa niaba ya wapiga kura wa Jimbo la Sengerema kuelezea faraja niliyonayo ya kupata msamaha, na naamini kuwa Mwenyezi Mungu atazidi kumjalia Mh Rais'' amesema Ngeleja.
Hatua hii imekuja ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais Magufuli, alipoamua kuwasamehe wabunge hao, akiwemo January Makamba na Nape Nnauye, mara baada ya kuvuja kwa sauti zao na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zilizosikika zikitoa maneno yasiyofaa dhidi ya Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list