Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kesho kuwashuhudia wachezaji wapya wa timu yao watakaposhuka dimbani kuikabili Kariobangi Sharks
Akizungumzia maandalizi ya mwisho baada ya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo, Zahera amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri
"Wachezaji wote wako katika hali nzuri hatuna majeruhi hata mmoja," amesema
"Ukiondoa wachezaji wachache ambao walichelewa kuanza mazoezi, wengine wote 'fitnes' yao ni nzuri"
"Kesho Wanayanga waje wengi sana uwanjani waonyeshe mapenzi kwa wachezaji wao wapya"
"Sababu wachezaji hawa wapya, mwaka huu nadhani watawafurahisha sana, hivyo nawaomba wote wanaoipenda Yanga waje kwa wingi uwanjani"

No comments:
Post a Comment