Kikosi cha Yanga kiko mkoani Kilimanjaro ambapo leo kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania
Mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Ushirika Moshi, ni maalum kuwandaa mabingwa hao wa kihistoria kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema atatumia michezo miwili ya kirafiki watakayocheza kuimarisha timu yake kabla ya kuwafuata Rollers
Mchezo huo utapigwa saa 10 jioni na utakuwa mbashara Azam Sport 2

No comments:
Post a Comment