Mlinda lango Klaus Kindoki anaondoka Yanga kumpisha mshambuliaji David Molinga ambaye pia ametua kutoka DR Congo
Kindoki alitua Yanga mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili, hata hivyo hatamaliza mwaka uliobaki baada ya makubaliano kufikiwa na uongozi wa Yanga kuwa ampishe Molinga
Hata hivyo mlinda lango huyo amesema hana kinyongo na uamuzi huo uliofikiwa, anaamini kuondolewa kwake ni kutokana na matakwa ya sheria ya idadi ya wachezaji wa kigeni na sio kwamba hana uwezo
Amesema ataendelea kuikumbuka Yanga hasa mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wakimuunga mkono nyakati zote
"Nitawakumbuka mashabiki waliokuwa wakinipenda na kuniunga mkono kila nilipocheza," amesema
Aidha Kindoki amesema anamfahamu vyema mshambuliaji Molinga 'Falcao' na anaamini mkali huyo wa kuzifumania nyavu atakuwa na mafaniko kwenye ligi ya Tanzania
Kuna taarifa kuwa Kindoki huenda akarejea klabu ya Fc Lupopo ambayo alikuwa akiitumikia kabla ya kusajiliwa na Yanga
Heritier Makambo aliyetimkia Horoya AC, Kindoki na Molinga wote wamewahi kucheza klabu ya Fc Lupopo

No comments:
Post a Comment