Waziri wa Madini Dotto Biteko ameiagiza Ofisi ya Madini Mkoani Kigoma kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuona uwezekano wa kuanzisha soko la madini ya chumvi Wilayani humo ili kutoa nafasi kwa wakazi hususani wa kipato cha chini kunufaika na rasilimali hiyo inayopatikana kwenye maeneo yao.
Ameyasema hayo Waziri Biteko Mkoani Kigoma ambapo yupo katika ziara ya siku mbili amekagua na kuongea na wachimbaji wadogo wa madini ya chumvi Wilayani Uvinza na wachimbaji wa madini ya chokaa Wilayani Kasulu ambapo ameuagiza Uongozi Wilayani Kasulu kuweka mazingira rafiki ya kumnufaisha mwananchi wa chini ili kuongeza pato.
No comments:
Post a Comment