Ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Agosti 2, 2019 mjini Bukoba baada ya kupokea taarifa ya Tasaf Mkoa wa Kagera.
Dk Mwanjelwa amesema malipo kwa kaya masikini yataanza kutolewa Agosti 2019 baada ya taratibu kukamilika.
Amesema Serikali imeridhia mpango wa Tasaf uendelee na kuwa awamu inayokuja ina maboresho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatambua walengwa kwa njia ya kielektroniki ili kuepuka kaya hewa.
Pia, amesema awamu inayofuata kaya masikini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi watatakiwa kufanya kazi za kuwaingizia ujira na kuwa mfumo ulioboreshwa utatatua changamoto zilizokuwepo likiwemo suala la kaya hewa.
Naibu Waziri huyo amesema mpango wa kunusuru kaya masikini umesaidia familia nyingi kupiga hatua na kuwa mabadiliko makubwa yanatarajiwa katika awamu ijayo.
Katika taarifa yake mratibu wa Tasaf Mkoa wa Kagera, Afraz Mukama amesema miongoni mwa changamoto hizo ni wingi wa kaya ambazo hazipo kwenye mpango hali inayosababisha manung'uniko na wengine kuhusisha na masuala ya kisiasa.

No comments:
Post a Comment