Watu watano wamefariki baada ya Gari la Dangote lililokuwa limebeba malighafi ya kutengenezea saruji likielekea Mtwara kugongana na Gari dogo na kupinduka kisha kuwaka moto baada ya kupoteza muelekeo na kugonga nguzo ya umeme ikaanguka na waya wenye moto ukanasa kwenye bodi ya gari hiyo ya Dangote ndipo watu wa 4 wakafariki papo hapo na mmoja aliyekuwa kwenye gari dogo akafariki wakati akipatiwa matibabu, wilayani rufiji mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amethibitisha tukio hilo ambapo ameeleza kuwa gari ndogo Toyota Premio ilikuwa ikitokea kwenye makazi ya nyumba za walimu wa sekondari ya Kibiti eneo la Kinyanya, ikiingia katika barabara kuu inayotoka Dar es Salaam kwenda Mtwara bila kuzingatia sheria na ndipo ikagongana na gari kubwa la Dangote.
Amesema gari la mzigo la Dangote lilipoteza muelekeo, likaelekea kulia zaidi mwa barabara na kutoka nje na kwenda kugonga nguzo ya umeme, wakati hiyo nguzo ya umeme inadondoka waya wa umeme ukanasa kwenye bodi ya gari na wote waliokuwepo kwenye gari hiyo ya Dangote waliteketea kwa Shoti hiyo ya umeme.
No comments:
Post a Comment