We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 2, 2019

Ujumbe wa Dk Mashinji kwa viongozi nchini Tanzania

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Vicent Mashinji amewataka viongozi nchini kutumia akili kuhakikisha utukufu wa Mungu unaonekana.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 2, 2019 wakati akitoa salamu katika misa ya mazishi ya Meja Jenerali mstaafu, Alfred Mbowe iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nshara Machame.
Alfred, kaka wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifariki dunia Jumapili Julai 28, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliagwa jijini Dar es Salaam Jumatano Julai 31, 2019 na  kusafirishwa kwa ajili ya mazishi yanayofanyika leo.
Amesema Alfred alitumia mwili wake, akili na roho kuhakikisha amani inakuwepo Tanzania, kwamba ni wajibu kwa waliopewa fursa ya kuongoza kutafakari na kuishi maisha kama ya Alfred.
"Haijalishi unaishi miaka mingapi duniani, ila umeacha alama gani kwa wale tuliopewa fursa ya kuongoza Taifa kwa namna moja ama nyingine. Tutumie akili zetu na miili yetu kuhakikisha utukufu wa Mungu unaonekana,” amesema Dk Mashinji


Amesema viongozi waliopewa dhamana kwa sasa wanapaswa kubadilika hasa wanapoona baadhi ya viongozi wametangulia mbele za haki.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list