Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa Twitter, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limebainisha kusudio la kupunguza idadi ya timu zinazoshiriki ligi kuu kutoka 20 mpaka 16 msimu wa 2021/22
TFF imeeleza kufikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini ya kina kuhusu mwenendo wa ligi yenye timu 20
Kuna uwezekano mkubwa misimu miwili ijayo, timu nne zitashuka daraja na timu mbili kupanda kutoka Ligi Daraja la kwanza
Moja ya changamoto iliyoikabili TFF msimu uliopita baada ya kuongeza idadi ya timu, ni kukosekana kwa Mdhamini wa ligi
Kampuni ya Vodacom iliyokuwa ikiidhamini ligi hiyo kwa zaidi ya misimu mitano ilijitoa
Msimu huu TFF imethibitisha kuwa ligi itakuwa na mdhamini na atatangazwa August 15

No comments:
Post a Comment