We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, August 5, 2019

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATATU

Barcelona imefutilia mbali uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Neymar, 27, kutoka Paris St-Germain katika dirisha hili la usajili. (Goal.com)
Manchester United wameafikiana kwa mkataba wa usajili wa mwaka mmoja wenye thamani ya £6.2m- na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33.
Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia huenda pia akafikia gharama ya karibu £15m au atakuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa United na Ubelgiji, Romelu Lukaku, 26. (Mail)

Romelu LukakuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRomelu Lukaku aliifungia United Mabao 15 msimu uliyopita

Real Madrid wameamua kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ajax, Mholanzi Donny van de Beek, 22, badala ya kung'ang'ania usajili wa Mfaransa Paul Pogba, 26 kutoka Manchester United. (Marca)
Leicester inatathmini uwezekano wa kumsajili James Tarkowski, 26, wa Burnley ama Nathan Ake, 24, wa Bournemouth katika safu yao ya ulinzi kuchukua nafasi ya beki wao Muingereza Harry Maguire, 26, ambaye anahusishwa na harakati za kuhamia Man United. (Sky Sports)

Harry MaguireHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mabingwa Manchester City wanajiandaa kukamilisha usajili wa £32m wa beki wa Ureno Joao Cancelo, 25, huku beki wa pembeni Mbrazil Danilo, 28, akitarajiwa kuondoka. (Mail)
Tottenham wanapigiwa upatu kumjumuisha Josh Onomah, 22, katika mkataba wao wa £30m kumsaini mlinzi wa Fulham Ryan Sessegnon, 19. (Mail)
Crystal Palace wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 25- Victor Camarasa - ambaye msimu uliopita alikuwa Cardiff kwa mkopo. (Independent)

Victor Camarasa akizungumza na kocha wa Cardiff Neil WarnockHaki miliki ya pichaHUW EVANS AGENCY
Image captionVictor Camarasa akizungumza na kocha wa Cardiff Neil Warnock

Watford wamekataa dau la £32m kutoka kwa Everton kumnunua kiungo wa kati wa miaka 26 Mfaransa Abdoulaye Doucoure. (RMC, via Express)
Mshambuliaji wa Brentford, Mfaransa Neal Maupay 22, anatarajiwa kujiunga na Brighton kwa kandarasi ya miaka minne. (L'Equipe - in French)
Brighton inatarajiwa kukamilisha usajili wa Maupay kwa fedha za juu katika rekodi ya klabu hiyo. (Talksport)

Wayne RooneyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWayne Rooney

Nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, anataka kurejea Manchester United kama kocha pale atakapostaafu kandanda. (Sun)
Rais wa Becelon Barcelona Josep Maria Bartomeu amegusia kuwa mabingwa hao wa Uhispania huenda wakafanya usajili mwingine baada ya kuthibitisha kuwasili kwa Junior Firpo, 22, kutoka Real Betis. (Sport)
Inter Milan imemwambia mshambuliaji wa Argentina, Mauro Icardi, 26, kuwa hatacheza kwa miaka miwili ikiwa ataendelea kusisitiza kusalia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapokamilika. (Gazzetta Dello Sport)

Mauro IcardiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMauro Icardi

West Ham wanapania kumsajili mchezaji wa tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini hawana mpango wa kumsaini mlinzi wa zamani wa Chelsea na kiungo wa kimataifa wa England Gary Cahill, 33. (Football.London)

Tetesi Bora Jumapili

Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)
Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)

Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany - in German)
Mchezaji wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPogba Pogba

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list