We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, August 4, 2019

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMAPILI

Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)
Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)
Mchezaji wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)
Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany - in German)

Winga wa Man City Leroy Sane

Sane anakabiliwa na uwezekano wa kupoteza £11m katika mshahara wake iwapo ataendelea kukataa kutia kandarasi mpya na Man City . (Sunday Mirror)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anapima uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco na beki wa Bournemouth Nathan Ake, 24. (Sunday Express)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco

Manchester United wamefanya mazungumzo ya kubadilishana wachezaji na Juventus ambapo mchezaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, na mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic wataelekea Old Trafford, huku naye mchezaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, akielekea Juventus. (Sunday Times - subscription required)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anataka kumsaini beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33 kwa mkopo wa miaka miwili. (Sun on Sunday)
Barcelona inajiandaa kuanza mazungumzo na PSG kuhusu kumununua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, back to La Liga. (Goal.com)

NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa manchester United ameambia klabu ya Sporting Lisbon kwamba anataka kujiunga na Tottenham. (Mail on Sunday)
Real Madrid wameafikia makubaliano na mchezaji mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uholanzi Donny van de Beek, lakini bado hawajakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo na klabu yake Ajax.. (Marca)
Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anapanga kumnunua beki wa Norway Kristoffer Ajer, 21 kwa dau la £21m. (Star Sunday)
Barcelona wameafikia makubaliano na Real Betis kumsaijili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 Junior Firpo kwa dau la £22m. (ESPN)

Junior FiripoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Burnley have joined Crystal Palace in the race to sign Real Betis' Spanish midfielder Victor Camarasa, 25, who spent last season on loan at Cardiff City. (Sky Sports)
Tottenham imejiandaa kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Ryan Sessegnon, 19, kutoka Fulham, lakini huenda ikamkosa kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 na Real Betis Giovani lo Celso kwa hatua hiyo. (Star Sunday)
Hatahivyo Spurs wanapigiwa upatu pamoja na Atletico Madrid kumsaini beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter, 25 kwa dau la £60m. (Bild, via 90min)

Beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter

Tottenham wako tayari kushinda na Roma pamoja na Juventus kumsajili beki wa kulia wa napoli na Albania Elseid Hysaj, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Chelsea msimu uliopita (Sunday Express)
Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anasema kuwa atamuomba mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuongeza wachezaji zaidi kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho siku ya Alhamisi na anasema kwamba anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Dwight Gayle, 28, kusalia katika klabu hiyo licha ya hamu kutoka klabu ya Leeds..(Newcastle Chronicle)
Leicester wameripotiwa kumlenga beki wa Getafe na Togo Djene Dakonam, 27, kujiunga na klabu hiyo ili kuchukua mahala pake beki wa Uingereza ambaye anataka kujhiunga na Man United Harry Maguire, 26. (Leicester Mercury)

Leicester wameripotiwa kumlenga beki wa Getafe na Togo Djene Dakonam,

Chelsea wako tauari kusikiliza ofa ya kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, na Uingereza Danny Drinkwater, 29. (Sunday Telegraph)
Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza Drinkwater anatakiwa na klabu ya Brighton kwa mkopo msimu huu. (Mail on Sunday)
Beki wa kushoto wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, 22, huenda akakosa hadi wiki nane kupitia jeraha na hivyobasi kumaliza hamu ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya £25m (Sun on Sunday)

Kierran Tierney

Mshambuliaji wa manchester City ambaye ni raia wa Ujerumani Lukas Nmecha, 20, atahudumu msimu 2019-20 kwa mkopo katika klabu ya Bundesliga ya bWolfsburg. (Manchester Evening News)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list