We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, August 25, 2019

SHULE YAPEPERUSHA BENDERA NYEUSI BADALA YA ILE YA TAIFA "TULISHIKA MKIA"

Shule ya Msingi Namlonga iliyopo kijiji cha Namlonga kata ya Manyara takribani kiliomita 45 kutoka makao makuu ya mkoa wa Songwe matokeo ya darasa la saba msimu wa 2018 ilishika nafasi ya mwisho kimkoa kati ya shule 420 na nafasi ya mwisho kiwilaya kati ya shule 161. Mkuu wa shule hiyo Hassani Mlilo amesema walipewa bendera hiyo waipeperushe na viongozi wa Halmashauri ya Mbozi kama fundisho kwa walimu na viongozi wa kijiji na kata kutokana na matokeo hayo mabaya ambayo hayajawahi ikumba shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1991. Amesema sababu zilizoifanya shule hiyo kushika nafasi ya mwisho katika orodha ya shule zote wilayani Mbozi na mkoani songwe kuwa ni pamoja na ushirikiano mbaya wa wazazi kwa walimu kuanzia kwa wanafunzi wa elimu ya awali mpaka darasa la saba, wanafunzi kutembea umbali mrefu na miundo mbinu ya madarasa na vyoo kuwa mibovu hali iliyopelekea mwalimu Mkuu kutumia muda mwingi katika kusimamia miundo mbinu hiyo baada ya fedha za serikali za kuboresha miundo mbinu shuleni hapo kuingia mwakajana . Mlilo amesema wameamua kujipanga ili kutoa bendera nyeusi ambayo wameipata kutokana na matokeo mabaya kwa kuboresha miundo mbinu ya vyoo ambayo ilikuwa kero kwa wanafunzi, kufundisha muda wa ziada , kuweka kambi wanafunzi ili kuwasimamia nyakati za usiku kuwafundisha na kujisomea. aliitaja sababu nyingine ambayo ni mpango wa muda mrefu kuwa ni kuboresha elimu ya awali kwa kuwaandalia vizuri watoto hao mazingira mazuri ya kujifunzia pamoja na vifaa vya kufundishia ambapo tayari wana mwalimu aliyepata mafunzo ya ufundishaji elimu hiyo. Meshack Gunza Mwenyekiti wa kijiji hicho alipohojiwa kuhusiana shule yao kupeperusha bendera nyeus amesema kuwa ushirikiano mbaya kati ya wazazi na walimu ndio chanzo cha shule hiyo kupata bendera hiyo nyeu ambayo wanaiona kama msiba. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Elick Minga amesema shule hiyo ilipewa bendera ikiwa ni ishara ya kuitaka ifanye juhudi ambazo zitapelekea kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba wa mwaka huu 2019. amesema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kutoa bendera nyeusi kwa shule zinafanya vibaya matokeo ya darasa la saba na kata zinazofanya vibaya lengo kubwa likiwa ni kuongeza juhudi kutokana na aibu ya bendera nyeus ambayo ni ishara ya kuonyesha kuwa umefel kwasabu huwekwa shuleni ili kila mtu aone .

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list