PSG inapanga kuwasilisha dau la £100m ili kumnunua winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wlfried Zaha 26 ili kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Brazil Neymar 27.(Sunday Mirror)
Manchester United inafikiria kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City James Morisson mwezi Januari ambaye anadaiwa huenda akagharimu£80m. (Sunday Mirror)
Manchester United na Inter Milan zitaendelea na mazungumzo siku ya Jumatatu kuhusu makubaliano ya mkopo wa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez. (Observer)
Watford inafikiria hatma ya mkufunzi wake Javi Gracia baada ya kuanza kampeni yao ya Premia baada ya kupoteza mara tatu na hivyobasi kushindwa mara saba mfululizo kutoka msimu uliopita.. (Mail on Sunday)
Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kipa wa Everton mwenye umri wa miaka 36 Maarten Stekelenburg iwapo mlinda lango wao raia wa Chile Keylor Navas, 32, atahamia PSG. (Football Insider)
United itafikiria kumsaini kipa wa Croatia Dominik Livakovic, 24, kwa dau la £20m kutoka Dinamo Zagreb iwapo raia wa Uhispania David de Gea, 28, hatotia saini ya mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Sun on Sunday)
Real Sociedad imekubali kumsaini beki wa Arsenal na Uhispania Nacho Monreal, 33. (Marca - in Spanish)
Tottenham wana matumaini kwamba beki wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 Toby Alderweireld atatia kandarasi mpya . (Sun on Sunday)
Fiorentina imejiunga katika harakati za kumsaini mshambuliaji wa Liverpool na Enlgand Bobby Duncan kwa mkataba wa msimu huu . (Mail on Sunday)
Paris St-Germain inajaribu kutatua haki za mauzo za Paulo Dybala huku wakitaka kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Argentina kutoka Juventus.(Calciomercato)
Southampton inamchunguza mshambuliaji wa QPR mwenye umri wa miaka 21 Eberechi Eze kabla ya uhamisho wa mwezi Januari . (Sun on Sunday)
Sampdoria ina hamu ya kumsaini kipa wa Aston Villa na Croatia Lovre Kalinic, 29. (Il Secolo XIX - in Italian)
Fifa inachunguza iwapo Roboti zinaweza kuchukua mahala pao marefa wa usaidizi ili kutoa maamuzi ya mipira ya kuotea kwa kuwa tayari wanasaidia katika VAR. (Sunday Mirror)
No comments:
Post a Comment