Apple, watengenezaji wa Iphone wamesema mwezi wa Tisa mwaka huu watatambulisha teknolojia mpya ya IOS 13 ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa Apps za Facebook, Whatsapp na zingine zinazotumia Internet (voice over internet protocol – VoIP).
Katika toleo hilo,iOS haitaruhusu apps zisizotumika kuendelea kufanya kazi kwa kificho(background) kwenye iPhone.
Apps zinazotumia teknolojia ya simu kwa njia ya intaneti kama vile Facebook na WhatsApp huwa zinaitaji apps hizo ziendelee kufanya kazi hata kama mtumiaji wa simu hazitumii kwa wakati huo.
Wao wanadai kwa kufanya hivyo ni rahisi zaidi mtumiaji kupata ujumbe anaotumiwa kwa wakati au kuunganisha haraka call anayopigiwa.
Uamuzi huu wa Apple umejikita zaidi katika suala la kulinda faragha ya watumiaji wa simu zake.
Apple wanadai kuwa bado apps hizo zikiwa zinafanya kazi nyuma ya pazia zimekuwa zikikusanya taarifa kuhusu utumiaji wa simu wa mtu bila ridhaa yake.
Watengenezaji apps wamepewa hadi Aprili 2020 kuhakikisha apps zao zinafuata utaratibu huu mpya.
Facebook kwa upande wao wamesema wapo katika majadiliano na Apple kuhusu utaratibu huu mpya.
No comments:
Post a Comment