We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 2, 2019

Ofisa wa TRA anaswa kwa kuomba rushwa ya mil 50

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Ilala inamshikilia Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya shilingi milioni 50 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba rushwa kwa mfanyabiashara raia  wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Heavy Equipments Company Ltd.
Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000.
Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000)'', amesema Ngailo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list