We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, August 5, 2019

NEC yatoa agizo kwa Vyama vya siasa


Jaji Mbarouk Salum Mbarouk ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ameviagiza vyama vya siasa nchini kuzingatia sheria za uchaguzi pamoja na kanuni za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema endapo agizo hilo litazingatiwa, uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani, utakuwa wa amani na utulivu.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa uchaguzi, Jaji Mbarouk alisema licha ya kuvitaka vyama vya siasa kuzingatia sheria za uchaguzi pia wadau wa uchaguzi wanapaswa kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wakati muafaka.

Amesema kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kuwa mpiga kura anapaswa kujiandikisha na mwenye kuhitaji kuboresha taarifa zake atumie nafasi hiyo kujitokeza ili kuboresha.

Alisema kwa upande wa Mkoa wa Mwanza, zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura litaanza Agosti 13, na litaendelea mpaka Agosti 19, mwaka huu.

Jaji Mbarouk amesema uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigaji kura safari hii halitahusisha wapiga kura wote walioandikishwa katika daftari la kudumu la mwaka 2015.

Alisema uboreshaji utawahusu wapiga kura wapya waliotimiza miaka 18 na wale watakaotimiza miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list