We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 21, 2019

Mkurugenzi ATCL aelezea Bombardier iliyoharibika


Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida.

Akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha  Clouds, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Ladslaus Matindi amesema taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha picha ya ndege hiyo ikiwa katika matengenezo.

“Ndege inaweza kuharibika, kupata hitilafu au kuingiliwa na kitu kutoka nje muda wowote kwakuwa ni mashine hakuna namna ya kuzuia hilo ni jambo la kawaida kwa mashine hata binadamu,” amesema Matindi.

“Ndege zinazoharibika sio za ATCL  pekee bali popote hata KLM ndege zao huwa zinaharibika, British Airways na Emirates wakisema ndege zao hazijawahi kuharibika ndipo tujiulize kwa nini zetu ziharibike.”

Aidha amesema kuwa ndege hiyo ipo Dar es Saalam tangu jana na matengenezo yake yalichukua siku moja, akibainisha kuwa yalianza Jumatatu mchana hadi jana mchana, “Usiku jana iliruka kurudi Dar es Salaam.”

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list