We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, August 20, 2019

Mke na mume watupwa Jela miaka 5 kwa kuwakeketa watoto wao watatu

Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela, Thadei Parokwa (43) na mke wake Lowema Thadei (34) kwa kuwakeketa watoto wao watatu. 


Mwendesha mashitaka wa Polisi mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Mkaguzi wa Polisi, Hamilton Moses, alisema shitaka lililowakabili washitakiwa hao kuwa ni ukatili dhidi ya watoto.

Amesema kesi hiyo iliripotiwa kituo cha Polisi Orkesmet tarehe Machi 19, mwaka jana baada ya kukamatwa watuhumiwa hao ambao walidaiwa kuwakeketa watoto hao kwa bibi yao aliyekuwa Kitongoji cha Kangala Kijiji cha Lobosireti Wilayani humo.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Lugano Kasebele, baada ya kujiridhisha kwa pande hizo mbili, aliwatia hatiani wazazi hao kwenda jela miaka mitano ama faini ya laki sita na fidia ya laki tisa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list