Miamba ya soka nchini Uingereza Manchester United ipo tayari kuwapatia Leicester City pauni milioni 80 kwaajili ya kumnasa beki wao kisiki Harry Maguire.
Kwa mujibu wa talkSPORT timu hiyo ya Leicester imepewa siku tano kuanzia leo, hadi ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo kuhakikisha inatoa majibu juu ya kukubaliana na ofa hiyo.
United inajaribu kutuma ofa ya pili baada ya ile ya kwanza ya dau la pauni milioni 70 kukataliwa na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza.
Hata hivyo Leicester walikuwa wanahitaji kuhakikishiwa wanapata dau nono la zaidi ya pauni milioni 75 ambayo mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya Liverpool waliipatia Southampton kwa mchezaji wao Virgil van Dijk.
Kama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa Harry Maguire atasajiliwa kwa pauni milioni 80 ambalo litakuwa limezidi lile la beki bora kwa sasa duniani Virgil van Dijk alipotua Liverpool kwa pauni milioni 75 na kuweka rekodi.
Alhamisi ijayo dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa, hivyo United inahaha kuhakikisha inamalizana na mchezaji huyo haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Maguire amemuambia kocha wake ndani ya Leicester, Brendan Rodgers kuwa anahitaji kwenda kujunga na United
No comments:
Post a Comment