Jana Jumapili, Yanga walihitimisha kilele chao cha Wiki Ya Mwananchi ambapo Manara amesema mambo yaliyofanyea na watani yao hayakwenda kisasa ikiwemo jinsi ya kutambulisha wachezaji.
"Kesho ndiyo shughuli yenyewe, nataka kuwaonyesha wenzetu na kuwafundisha jinsi ya kutambulisha wachezaji.
"Kesho ndiyo shughuli yenyewe, nataka kuwaonyesha wenzetu na kuwafundisha jinsi ya kutambulisha wachezaji.
"Wamefanya shughuli yao lakini hawawezi kutufikia hata robo, shughuli ipo kwetu hapo kesho (Jumanne),"amesema Manara
Kesho Simba wanahitimisha siku yao ya Simba ambayo hufanyika kila mwaka ikiwa ilianzishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wao Hassan Dalali.
Asha Baraka wanawake zaidi Simba
Katika hatua nyingine Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Asha Baraka ametaka ongezeko la wanawake ndani ya klabu hiyo.
Asha ameelezea hayo wakati akijitambulisha mbele ya Waziri aa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Dk Mwakyembe ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi aa uwekeji wa jiwe la msingi kwenye uwanja wa simba uliopo Bunju B.
Asha amesema "Mwakani tunataka Simba iwe na wanawake wengi kuliko wanaume, hilo linawezekana na itakuwa hivyo,".
Baada ya kutamka hayo wanawake waliofika kwenye shughuli hii walishangilia kwa nguvu wakionyesha kukubaliana na kauli ya mjumbe wao.

No comments:
Post a Comment