We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 28, 2019

Makonda aja na jipya kuhusu watoto wa nje ya Ndoa

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda, amesema atawasilisha muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya mirathi na sheria ya Ndoa kwa Waziri wa Katiba na Sheria, ili ziweze kufanyiwa marekebisho kutokana na sheria hizo kupitwa na wakati.

Makonda ameongeza kuwa sheria hizo zimeonekana kuwa kandamizi kwa wanawake wengi zaidi, hasa kile kipindi mwanaume anapofariki, jambo linalopelekea mateso na manyanyaso kwa wajane.
"Sheria kandamizi zinazotakiwa kufanyiwa mabadiliko ni sheria ya Kiserikali ya mirathi, sheria ya mirathi ya kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya kidini ya Mwaka 1963'' amesema Makonda.
Aidha Makonda ameshauri mara baada ya sheria kufanyiwa maboresho iweze kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, pamoja na usawa wa  watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja na haki ya mtoto wa nje ya ndoa kurithi Mali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list