Ikiwa ni wiki 12 zimepita tangu maandamano yaanze Hong Kong, Bado hakuna ishara yoyote ya maandamano hayo kumalizika kwani wananchi wanaopigania haki zao, Baadhi yao wamepanda katika milima ya Lion Rock na kuwasha Taa nyakati za usiku.
Maelfu ya waandamanaji wamesema kuwa wamepanda milimani, Ili kukimbia mateso wanayofanyiwa na maafisa usalama huku wakisikika wakiimba “TUPENI DEMOKRASIA AU TUUWENI”.
Maafisa wa usalama wa China, Wamesema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwatawanya mamilioni ya waandamanaji waliokuwa karibu na uwanja mkubwa wa michezo wa Kwai Chung, na wale waliokuwa katika daraja linalounganisha China bara na Hong Kong.
Tayari watu 29 wameshakamatwa na jeshi la Polisi huku mamilioni ya waandamanaji wakimwangiwa maji ya washawasha na kupigwa mabomu ya machozi.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, Baadhi ya familia za Maaskari Polisi zimeungana na waandamanaji Mjini Hong Kong.
Baadhi ya wachambuzi wanasema uwepo wa wanajeshi katika kutuliza ghasia za maandamano ni ishara ya ujumbe kutoka kwa Serikali ya Beijing kwamba ipo tayari kutumia nguvu kuvunja maandamano ya kudai mabadiliko ya demokrasia, Hong Kong.
Wakazi wa Hong Kong wamekuwa wakiandamana kwa wiki 12 sasa wakidai kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yao na Hong Kong kuingiliwa na China bara katika masuala ya jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment