Kikosi cha Simba saa kumi jioni kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili UD Songo ukiwa ni mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya kufanikiwa kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza, leo Simba inahitaji matokeo yoyote ya ushindi ili iweze kusonga mbele
Rekodi zake inapocheza uwanja wa Taifa zinaibeba Simba kwenye mchezo huo
Pamoja na kuwa na kikosi bora, mashabiki wake ni silaha muhimu zaidi, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa leo
Baada ya Azam Fc na Yanga kufanikiwa kusonga mbele jana, hakuna shaka, leo simba ina kila sababu ya kushinda na kujihakikishia nafasi ya kutinga raundi ya kwanza
Kila la kheri Simba...!!
No comments:
Post a Comment