We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 24, 2019

Maalim Seif apigwa 'stop' Temeke

Chama cha ACT - Wazalendo kimethibitisha kukamatwa na Jeshi la polisi  kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo Katibu wa kamati ya uadilifu Mbarala Maharagande, wakati wa harakati za uzinduzi wa matawi katika Kata ya Azimio Wilaya ya Temeke.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Agosti 24,  Katibu Msaidizi wa kamati ya itikadi, uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ATC Seif Suleimani, amesema Jeshi la polisi lilifika na kumzuia Mshauri Mkuu kufanya uzinduzi.
''Jeshi la polisi kutuzuia kufanya shughuli zetu kuu za msingi za kisiasa ni kutuingilia NA kuingilia uhuru wetu wa chama cha siasa, na tunalitaka jeshi la polisi mara moja liache kutuingilia katika kufanya shughuli zetu za kisiasa'' amesema Seif.
Aidha kiongozi huyo amesema chama hicho kinafanya shughuli ya uzinduzi wa matawi mapya ikiwa ni hatua ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa kama vyama vingine vya siasa vinavyofanya.

@ACTwazalendo
kimeeleza kuwa Polisi Temeke wamezuia kikao kilichokuwa kihutubiwe na Mshauri wao Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika ofisi ya ACT kata ya Azimio. Wanachama wameamriwa kutawanyika huku Katibu wa kamati ya uadilifu ya chama Maharagande Mbarala akikamatwa.

View image on TwitterView image on Twitter

See East Africa TV's other Tweets

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list