Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kwenye mchezo wa kesho dhidi ya UD songo wachezaji Ibrahim Ajib, Wilker Da Silva na John Bocco hawatakuwa sehemu ya kikosi
Wakati Ajib na Wilker wakirejea hivi karibuni baada ya kupona majeraha, Bocco bado majeruhi
Akizungumzia mchezo huo, Aussems amesema kikosi kiko tayari kupata ushindi
"Tuko tayari, tunafahamu tunahitaji kushinda mchezo huu. Tutafanya kila linalowezekana ili tuweze kupata ushindi" amesema
"Wachezaji wanafahamu mazingira ya mchezo huu. Unajuwa wakati mwingine matokeo ya 0-0 yana changamoto yake unapocheza nyumbani"
"Tumeona jana jinsi KMC walivyopoteza mchezo dhidi ya AS Kigali, tunahitaji kuwa makini sana kwani tunacheza na timu nzuri"
"Hautakuwa mchezo mwepesi lakini tutapambana. Kuwakosa Ajib, Da Silva na Bocco ni tatizo lakini nawaamini wachezaji waliopo, wataweza kutupa matokeo tunayohitaji"
No comments:
Post a Comment