Aliyekuwa kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko, amewashukuru viongozi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti aliyopata wakati wote aliocheza Yanga
Kamusoko aliyeichezea Yanga kwa misimu minne, amejiunga na klabu ya ZESCO United ya Zambia
"Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru viongozi, wanachama na mashabiki wa Yanga kwa kuweza kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu ndani ya miaka minne," amesema
"Najisikia furaha kucheza moja ya timu kubwa ukanda wa Afrika Mashariki. Nawatakia kila la kheri katika msimu mpya"
"Asanteni sana, natumaini tutakutana tena siku nyingine"
Kamusoko alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia ZESCO United inayonolewa na kocha George Lwandamina ambaye aliwahi kuinoa Yanga kwa msimu mmoja na nusu
Aliondoka mwishoni mwa msimu wa 2017/18 kurejea ZESCO

No comments:
Post a Comment