We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, August 29, 2019

Kaburi kubwa zaidi la watoto waliotolewa kafara lagunduliwa

Wanaakiolojia nchini Peru wamegundua kile kinachoaminika kuwa ni kaburi kubwa zaidi duniani la pamoja la watoto ambao walitolewa kafara na jamii yao.
Miili 227, ya kati ya miaka mitano mpaka 14 iligunduliwa karibu na mji wa pwani wa Huanchaco, kaskazini mwa mji mkuu wa Peru wa Lima.
Watoto hao inaaminika walitolewa kafara miaka 500 iliyopita.
Ugunduzi wa safari hii umekuja mwaka mmoja baada ya kugundulika makaburi yenye miili 200 ya watoto katika sehemu mbili tofauti nchini humo.
Wanaakiolojia wameliambia shirika la habari la kimataifa la AFP kuwa baadhi ya miili iliyofukuliwa hivi karibuni ilikuwa ingali na nywele na ngozi.
Watoto hao wanaonesha dalili ya kuwa waliuawa katika msimu wa mvua, na walizikwa mkabala na bahari ili kuwaridhisha miungu ya kiasili ya ChimĂș.
Haina uhakika wa moja kwa moja mauaji hayo yalitokea.
Jamii ya ChimĂș imeishi kaskazini ya pwani ya Peru na ilikuwa ni moja ya jamii zenye nguvu gani zaidi. Jamii hiyo ilikuwa na nguvu zaidi kati ya mwaka 1200 na 1400 kabla ya kupigwa na jamii ya Incas, ambao nao baadae walitawaliwa na Wahispania.

Remains of one of 227 children allegedly offered in a sacrificeHaki miliki ya pichaAFP

Walikuwa wakiabudu mungu mwezi waliemuita Shi ambaye waliamini ana nguvu kuliko jua. Waumini walikuwa wakitumia kafara ya watu hususani watoto kila walipokuwa wakifanya ibada.
Ufukuzi wa makaburi ungali unaendelea kwenye eneo hilo na wanaakiolojia wanaamini huenda miili zaidi ikagunduliwa.
"Ni kitu ambacho hakidhibitiki, hiki kitu cha makaburi ya watoto," mwanaakiolojia mkuu ameiambia AFP. "Kila unapochimba, kuna mwili mwengine".
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list