We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, August 3, 2019

Jezi mpya Yanga zaibua timbwili klabuni


PATASHIKA limezuka Makao Makuu ya Klabu ya Yanga baada ya mashabiki zaidi ya 100 kufurika wakitaka kununua jezi huku jezi hizo ikidaiwa zimemalizika.

Jana Ijumaa baadhi ya mashabiki walinunua jezi eneo hilo  zoezi la uuzaji  lilitakiwa kuendelea leo Jumamosi lakini matokeo yake mashabiki wamefika jezi hakuna.

Mtandao MCL Digital huu umeshuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa vikundi vikundi ukijadili kukosekana kwa jezi hizo na kuwatupia lawama viongozi na Kampuni ya GSM ambayo imepewa tenda ya kutengeneza jezi.

"Yaani inasikitisha watu tupo hapa tangu alfajiri kwa lengo la tununue jezi kesho (Jumapili) tuvae uwanjani lakini mpaka sasa saa 5 asubuhi hii hakuna jezi na viongozi wamejichimbia ndani hakuna majibu wanayotupa"alisema shabiki aliyefahamika kwa jina la Sadick Said.

Shabiki mwingine maarufu Ras Yanga amesema alitegemea jezi zingekuwepo nyingi ili mashabiki wanunua na kesho uwanja mzima upambwe kwa rangi za jezi mpya za kijani na njano lakini anashangaa jezi hamna.
"Yaani hata hatujui tatizo nini, tumezunguka sehemu nyingi jezi hakuna, hapa makao makuu ya Klabu ambapo tulitarajia tungepata jezi napo hakuna sasa inashangaza.

"Kinachoonekana watu wachache wamenunua jezi nyingi jana na sasa wanataka kuuza kwa kulangua kwani nasikia jana kuna baadhi wamenunua jezi hapa makao makuu halafu wanauza moja hadi  Sh 70,000," amesema.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list