We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, August 20, 2019

Huu Ndo Mti Mrefu Zaidi Kuliko Yote Duniani

WANASAYANSI nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100.

Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja la watafiti kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita.

Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walitumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio.

Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah,  umepewa jina la Menara ambalo linamaanisha jumba refu.
Mkweaji miti kutoka eneo hilo, ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba,  alisema alliogopa kuupanda mti huo.

”Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri sana. Sijui cha kusema, isipokuwa tu  hilo lilikuwa tukio zuri sana”, aliongezea.


Daktari Doreen Boyd, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa ugunduzi huo ulikuwa muhimu kwa kuwa ni sayansi inayosema miti kama hii inapatikana, ni mirefu, jambo ambalo hatukuwahi kudhani na huenda kuna miti mirefu zaidi ambayo haijagunduliwa.
”Hali hii inatukumbusha kwamba tunahitaji kuilinda miti,” alisema.

Daktari Alexander Shenkin, kutoka chuo kikuu cha Oxford , alisema baada ya kusikia ugunduzi huo walitembea kwa muda wa saa tatu hadi Menara.
Alisema: “Nimeona kile ambacho wanasema ni miti mingi, lakini nilipotembea hadi katika mti huu ambapo kichwa changu kilizidi kuangalia juu unapokaribia kileleni. Sijawahi kuona mti mrefu kama huu,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list