Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Chuo cha Ushirika wilayani Moshi
Wachezaji wa Yanga waliuanza mchezo huo taratibu wakionekana kutatizwa na hali ya uwanja na waliruhusu bao la mapema tu kwenye dakika ya tano kupitia mkwaju wa penati uliofungwa na Marcel Kaheza baada ya beki Mustapha Suleyman kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari
Bao la pili la Polisi lilipatikana kwenye dakika ya 74 mfungaji akiwa Ditram Nchimbi aliyetumia makosa ya Jaffar Mohammed ambaye alishindwa kuondoa mpira uliokuwa unaelekea langoni
Yanga ilikosa nafasi kadhaa, nafasi muhimu ikiwa mpira wa adhabu uliopigwa na David Molinga ambao ulichezwa na mlinda lango wa Polisi
Kwenye mchezo huo kocha Mwinyi Zahera alitumia kikosi tofauti na kile kilichocheza mchezo dhidi ya Township Rollers pengine akiweka tahadhari kwa wachezaji hao kuepuka majeraha
Yanga itashuka tena dimbani keshokutwa mkoani Arusha kuumana na AFC Leopards
Zahera amesema wachezaji ambao hawakupata nafasi leo, watacheza mchezo huo

No comments:
Post a Comment