Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe leo amezindua viwanja vya mazoezi vya klabu ya Simba Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es saalam
Katika eneo hilo Simba itakuwa na viwanja viwili vya mazoezi, kimoja cha nyasi bandia na kingine nyasi asili
Pia kutakuwa na kituo cha Michezo
Hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi imehudhuria na viongozi wa waandamizi wa klabu ya Simba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji 'Mo' na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori
Mashabiki wa Simba nao walijitokeza kwa wingi

No comments:
Post a Comment