We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, August 28, 2019

Chanzo cha kifo, mtoto aliyekanyagwa na bomba

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kiyungi iliyopo Manispaa ya Tabora mkoani Tabora, amefariki dunia mara baada ya kukanyagwa na bomba kubwa la maji huku mwingine akijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa akizungumza leo Agosti 28 na EATV & EA Radio Digital, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amedai kuwa mabomba hayo ni ya mradi mpya wa usambazaji wa maji mkoani humo kutoka Ziwa Victoria, yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye kiwanja cha shule hiyo.
''Mimi nipo eneo la tukio ambapo bomba la maji limeporomoka, lakini mpaka sasa hivi mmoja amefariki na mwingine ni majeruhi na amewekwa ICU. Hii ni ajali ambayo imewapata watoto wawili nafikiri walikuwa wanayachezea yakaporomoka'', amesema Kamanda Mwakalukwa.
Kamanda Mwakalukwa amelitaja jina la mtoto aliyefariki kuwa ni Paul Moses Mlyambula, ambapo majeruhi wa ajali hiyo amelazwa katika Hospitali ya mkoa ya Kitete kwa ajili ya matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list