Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewataka mashabiki kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu
Akizungumza katika mazoezi yaliyofanyika jana uwanja wa Gymkhana, Aussems alisema anajuwa huu ni wakati mgumu kwa kila Mwanasimba baada ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Hata hivyo hawapaswi kuruhusu matokeo hayo yavuruge mipango mingine waliyojiwekea ambayo ni kutwaa taji la ligi kuu na FA
"Najua mashabiki wanavyojisikia, ni hali ambayo pia imetukumba sisi benchi la ufundi pamoja na wachezaji," alisema
"Tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja ili waweze kurejea katika hali ya kawaida"
"Tumesahau matokeo hayo, sasa tunawajibu wa kukamilisha malengo yetu ya kutwaa mataji hayo mawili, tuna kikosi imara, tutaweza kufanikisha"
"Muhimu ni kwa mashabiki wetu kuwa nasi, wakati huu mgumu, wasituache, waendelee kutuunga mkono"
Kesho Alhamisi Simba itashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuchuana na JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu

No comments:
Post a Comment