Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Baker Kasumba (21), ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka kazini kuelekea nyumbani katika eneo la Kalerwe, Jijini Kampala siku ya Alhamisi ya Agosti 29, 2019 ya wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mjini Kalerwe, Imeeleza kuwa Kasumba alikutwa amepigiliwa misumari ya nchi 6 kwenye mikono yake yote katika makutano ya barabara ya Kalerwe.
Taarifa hiyo, inaeleza kuwa kijana huyo alivaa kofia ya Chama cha Tawala cha National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni.
Kwenye maelezo yake aliyoyatoa katika kituo kidogo cha Kibe mjini Kampala, Kasumba amesema kuwa wakati akiwa njiani kutoka kazini, Alisimamishwa na watu wawili na kisha walimvua kofia na kumvuta mikono yote miwili na kuanza kumpigilia misumari kwenye mikono yake, Huku wakimwambia ‘Kofia yako imekuponza’.
Polisi nchini Uganda inaendelea na uchunguzi kuwabaini watu hao waliomshambulia kijana huyo, Kwa sababu za kisiasa.
No comments:
Post a Comment