We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 16, 2019

Ajali ya Basi na Lori Yaua Watu Wanne Morogoro

Watu 4 wamefariki dunia na wengine 26,  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria na Lori  kugongana uso kwa uso katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU na Lori.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yakebila kuchukua taadhari.

"Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa August 16, saa saba na nusu usiku imetokea ajali eneo la Nanenane, Morogoro, basi mali ya kampuni ya Safari Njema ambayo ilikuwa inatokea DSM kwenda Dodoma imegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu 4 wamefariki.

"Ingawa watu 4 wamefariki ila abiria wengine waliokuwa kwenye basi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro sababu ya mshtuko na wengi wametibiwa na kuruhusiwa, wamebakia abiria 3 wanaendelea na matibabu, dereva wa lori ni miongoni mwa waliofariki.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo". Amesema Mutafungwa

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list